Unable to start

The following failed to load:

Please refresh to try again

Kutengeneza Chupi Kutoka kwa T-shirt – Hatua kwa Hatua

MAELEKEZO KWA MKUFUNZI (FACILITATOR NOTES)

1. Kabla ya Kuanza

  • Usiendelee kukata au kushona bado

  • Anza kwa kuonyesha kila hatua polepole, kwa mfano hai wa mchakato

  • Hakikisha kila mtu ameona hatua kabla ya kazi kuanza

  • T-shirt moja inaweza kutengeneza chupi za kujikinga + vitu vingine pia

  • Panga kwanza — usikate kiholela

2. Maandalizi na Kukata T-shirt

  • Tandaza t-shirt yote iwe tambarare (flat)

  • Kagua upande wa mbele na wa nyuma

  • Panga kabla ya kukata — weka sehemu za pattern mahali panapofaa kwanza

  • Kata mshono wa pembeni (side seams) wote hadi ifunguke kabisa

  • Hifadhi mikono ya t-shirt (sleeves) — ina kitambaa muhimu cha ziada

3. Kuchorea kwa Usalama (Bila Kuaharibu Meza)

  • Funika meza kwa plastiki au faili la plastiki

  • Tumia nukta ndogo ndogo, si mistari mirefu ya kalamu (inahifadhi wino na ni rahisi zaidi)

  • Unapokata, kata ndani kidogo ya nukta ili wino usionekane kwenye chupi ya mwisho

  • Chupi iliyomalizika haitakuwa na alama ya kalamu

4. Kuunganisha Mbele + Nyuma (“Good to Good”)

  • Weka sehemu ya mbele na ya nyuma uso mzuri kwa uso mzuri (good side touching good side)

  • Shona sehemu ya curve ya kati tu — acha nafasi ya mshono ya 1 cmBaada ya kufungua, uso mzuri utakuwa upande wa nje

5. Kutengeneza Tabaka la Ndani (Gusset ya Kujikinga)

  • Tumia kitambaa cha kuzuia maji (waterproof) au taulo kama sehemu ya ulinzi (core)

  • Weka core katikati ya kitambaa cha pamba (cotton top)

  • Kitambaa cha pamba lazima kiwe 1 cm kubwa kuzunguka kote

  • Shona kingo za juu (waterproof + cotton) karibu na ukingo

  • Vuta sehemu ya waterproof hadi ukingo wa chini na uishone pia karibu na ukingo

  • Geuza upande (turn inside out) — kingo za juu na chini ziwe safi

  • Shona tena kando ya ukingo wa curve wa waterproof ili ibaki tambarare na isimame vizuri juu ya cotton

6. Kuweka Mikanda ya Usalama (kwa pad/liner)

  • Kata mikanda kutoka kingo za chini za t-shirt (hem), geuza ndani kupata upana wa ½ cm

  • Mbele = umbali wa vidole 2 kutoka juu

  • Nyuma = umbali wa vidole 3 kutoka nyuma

  • Nafasi ya kuingiza pad/liner = vidole 4

  • Umbali kati ya mikanda ya mbele na nyuma ≈ urefu wa kiganja kimoja

  • Shona kwa usalama, ongeza kushona mara mbili upande wa nyuma ili liner isipotele au kuteleza wakati wa kuvaa

7. Kuunganisha Gusset — “Good to Good”

  • Weka sehemu nzuri ya gusset (ambayo ina mikanda) kwa uso mzuri wa chupi

  • Hakikisha curve ya gusset inafuata curve ya mguu ya chupi sawasawa

  • Shona ndani ya nafasi ya mshono ya 1 cm pekee — usishone juu ya sehemu ya waterproof

  • Vuta gusset hadi upande wa pili wa mguu na urudie

  • Geuza upande (turn inside out) — sasa gusset iko ndani ya chupi

8. Kufunga Pembeni + Kumalizia Kiuno (Bila Elastic)

  • Shona pande zote mbili — ukiacha nafasi ya mshono ya 1 cm

  • Fungua mshono upande wa ndani na uulaze (usipindishe upande mmoja)

  • Pinda kiuno chini kwa urefu wa kidole gumba kimoja

  • Shona nusu sentimita pembeni ya mshono hadi chini, geuza, urudi juu upande wa pili

  • Hakuna elastic inayohitajika — muundo huu hukaa vizuri kwenye nyonga

9. Mwisho

  • Hakiki kuwa nje ni laini na ndani ni safi

  • Chupi ni rahisi kuvaa, hudumu, inafuliwa, na salama

Wahimize washiriki kufundisha wengine pia — ni ujuzi unaoleta heshima na matumaini


FACILITATOR NOTES 

1. Before Starting

  • Do not start cutting or sewing yet

  • First show each step slowly with process sample

  • Make sure everyone sees the process before action begins

  • One t-shirt can make protective underwear + other things

  • Plan first — no random cutting

2. Preparation & Cutting from T-Shirt

  • Lay the whole t-shirt flat

  • Check front and back

  • Plan before cutting — place pattern pieces first

  • Cut side seams completely to open the shirt flat

  • Keep sleeves — they are useful extra fabric

3. Tracing Safely (Without Damaging the Table)

  • Protect the table with plastic or folder 

  • Do small dots — not long marker lines  (Easier & saves ink)

  • When cutting, cut just INSIDE the dots so no ink shows on finished product

  • Final underwear will then have no marker showing

4. Join Front + Back (Tip: Remember keep sides “Good to Good”)

  • Place front + back pieces face to face (good side touching good side)

  • Stitch only the middle curve — 1 cm seam allowance

  • Open the joined pieces,  now the good side is on the outside

5. Make the Inner Protective Gusset

  • Use waterproof or towel fabric as the core

  • Place core centered on cotton top piece

  • Cotton must be 1 cm bigger all around

  • Stitch both top edges together (waterproof & cotton) close to the edge

  • Pull waterproof  to the other bottom edge of cotton — stitch together close to the edge

  • Turn inside out — top and bottom have a clean edge

  • Now stitch along the open curved edge of waterproof to keep it flat and secured to cotton layer

6. Attach Security Bands (for pad/liner)

  • Cut bands from t-shirt hem (turn hem inside out to get ½ cm band)

  • Front band = 2 fingers from top

  • Back band = 3 fingers from back

  • Space between reinforcing stitches = 4 fingers 

  • (this is where the liner will go between the bands)

  • Space between front and back bands ≈ one hand length

  • Attach bands to edge with reinforcing stitches, for the back band, adding additional reinforcing stitches to accommodate only the 4 fingers space for liner will prevent liner shifting during wear

7. Attach Gusset - “Good to Good”

  • Put good side (gusset with bands)  to good side (outer face) of underwear

  • Ensure placement of the gusset follows the underwear’s leg curve

  • Ensuring the cotton gusset layer and the underwear leg curves are matching together, stitch together, but avoid stitching through the waterproof part of gusset

  • Then pull the gusset to the other leg curve and repeat

  • Turn inside out — now the gusset is on the inside of underwear

8. Close Sides + Finish Waist

  • Sew side seams — 1 cm width seam allowance

  • Open seam flat inside (no folding to one side)

  • Fold waist down 1 thumb-length down

  • Sewing 1/2 cm beside the seam down, turn at bottom, and back up the other side

  • No elastic needed — hip fit design

  • Side Seams & Waistband Finish

  • Sew side seams using a 1 cm seam allowance.

  • Open and flatten the seam for a smooth, professional finish.

  • Fold the waistband down using one thumb-length as the measuring guide.

  • Stitch down and back up again to fully secure the waistband.

9. Finish

Confirm smooth outside and clean inside

Underwear is comfortable, durable, washable, safe

Encourage sharing and training others with this skill, as it brings dignity and hope.




Patterns Courtesy of Transformation Textiles. Used with Permission. 

All are free to share widely with any person who would like a copy.

TT Hipster XS.pdf

TT Hipster S.pdf

TT Hipster M.pdf

TT Hipster L.pdf

TT Hipster XL.pdf

TT Hipster 2XL.pdf

TT Hipster 3XL.pdf

TT Hipster 4XL.pdf

TT Hipster 5XL.pdf



Comments